Mobi Groups
Download Free Apps & Games @ PHONEKY.com

SwahilihiphopEA - Topics
Create Your Own App Store

* SwahilihiphopEA > Topics


Subject: Karibu kwenye michano!
Replies: 1 Views: 876

krity 20.08.10 - 01:48pm
Karibu kwenye michano,ni kijani twende si nyekundu wala njano,onyesha mshikamano,ka santuri na sindano,hiphop halisi wala si mfano,hizi si hadithi wala si tungamo,watunzi wachovu nawapa kibano,huwezi huu mpambano kitungo mi nna makamo,nawavuta na kuwapuliza kama sigara,ka usingizi nawalala,mi ni mkuna nawapoza harara,kama kamari nawapuna kama msosi nawala,mi ni mtemi natawala,nawakimbiza masakala,mi kimbunga nawatawanya mi onyo nawakanya,ka mkutano nawakusanya,wao hasi mi chanya,mie paka wao panya,huu ni kama tu muhtasari wa habari,mistari hii ni hatari,kaa chonjo kaa mbali,ajibu mwenye mistari... *

shafftan 21.08.10 - 11:51am
Tungo zako za kitoto unaimba utoko,unataka pambana,huwezi we hata na wako wana,nakuanika kweupe mchana,unachana ka msichana,we wa makamo mi kijana,ndo maana nna uwezo sana.. *


* Reply
* SwahilihiphopEA Forum


Search:
topics replies


* SwahilihiphopEA

Create Your Own App Store

topTop
groupsGroups
mainProdigits

Create Your Own App Store